Neno Down Syndrome limetokana na jina la mtu wa kwanza, aliyegundua hali hii, kwa jina Langdon Down. Alikuwa tabibu (physician) Mwingereza.

Huu ni mpangilio wa chembechembe (kromosomu) ambavyo ni sehemu ya hali ya binadamu ambayo huweza kutokea kwa watu wa aina zote bila kujali rangi, jinsi, wala hali ya kiuchumi ya mtu.

Kwa taarifa za Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Down Syndrome humpata mtoto mmoja (1) kwa kila watoto mia nane (800) wanaozaliwa duniani kote na huathiri ukuaji wa mwili na kiakili na hivyo huhusishwa na kuwa ni suala la kitabibu zaidi. Muonekano na hali ya athari za ufahamu: Watoto wanaozaliwa na hali ya Down Syndrome mara nyingi huwa na hali ya kufanana.


Wanakuwa na ulimi mkubwa uliotokeza nje, uso tambaa, shingo fupi na namuonekano wa vidole vya miguu na na mikono ni tofauti kama inavyoonyeshwakwenyepicha.
Nini husababisha mtoto kuzaliwa na hali ya Down Syndrome? Down syndrome husababishwa na chembechembe zinazoitwa chromosomes. Kwa kawaida binadamu huwa ana chromosomes 46 lakini watu wenye Down Syndrome huwa na chromosomes 47. Kuwa na zaidi ya chromosomes hubadilishwa mfumo wa jinsi ya ukuaji wa ubongo na mwili wa mwanadamu.

Down syndrome ni hali(sio ugonjwa) anayokuwa nayo mtu kwa maisha yake yote. Panapokuwa na huduma na msaada bora watoto wenye hali ya Down syndrome wanaweza kukuwa wakiwa na afya, furaha na kuleta tija katika jamii wanayoishi.

Watu wa hali ya Down Syndrome wako wangapi Tanzania? Tanzania Bara hakuna takwimu za watu wenye hali ya Down Syndome kwani hadi sasa hakuna tafiti zilizofanyika kujua ukubwa wa tatizo hili.